us-doj-guidance-CRT-1316146•Information for Refugees and Asylees About the Form I-9 (Swahili)
Information for Refugees and Asylees About the Form I-9 (Swahili)
us-doj-guidance-CRT-1316146Information for Refugees and Asylees About the Form I-9 (Swahili)Guidance
Maelezo ya Wakimbizi na Wahamaji Kuhusu Form I-9 Kila mtu anayeanza kazi kama mfanyakazi nchini Marekani hujaza Form I-9, fomu ya serikali ambayo waajiri hutumia kuthibitisha utambulisho wako na ruhusa ya kufanya kazi. Maelezo haya yamekusudiwa kukusaidia wewe, wahamaji na wakimbizi, kujaza Form I- 9 na kujua haki zako. Waajiri wanaokubagua kulingana na uraia wako, hali ya uhamaji au asili ya kitaifa wakati wa mchakato wa Form I-9 wanaweza kukiuka sehemu ya Sheria ya Uhamaji na Uraia (Immigration and Nationality Act, INA). Sheria hii ya kupinga ubaguzi inapatikana kwenye 8 U.S.C § 1324b. Kukamilisha Form I-9 Kwa Section 1 ya Form I-9, toa maelezo kukuhusu. • Weka jina lako na maelezo mengine kukuhusu katika Section 1 ya Form I-9. o Unaweza kumwomba mtu akusaidie kujaza sehemu hii. • Ni lazima utie alama kwenye kisanduku kinachoonyesha hali inayokupa ruhusa ya kufanya kazi. o Wakimbizi na wahamaji wanapaswa kuweka tiki kwenye kisanduku cha nne cha "A noncitizen authorized to work" (Mtu asiye raia aliyeidhinishwa kufanya kazi). Sehemu ya Haki za Wakimbizi na Wafanyakazi justice.gov/ier Maelezo ya Wafanyakazi Idara ya Haki ya Marekani Divisheni ya Haki za Kiraia
Kuna nafasi ya kuweka tarehe ya mwisho wa matumizi, ikiwa ipo, kando ya kisanduku hiki. o Kwa sababu muda wa haki yako ya kufanya kazi hauishi, andika "N/A" (ambayo ina maana "haitumiki") katika nafasi ya tarehe ya muda kuisha. Kwa Section 2 ya Form I-9, onyesha hati za mwajiri wako zinazoonyesha utambulisho wako na ruhusa ya kufanya kazi. • Form I-9 ina orodha tatu za hati ambazo unaweza kuonyesha kwa Section 2 ya Form I-9: o List A (hati zinazoonyesha utambulisho wako na ruhusa ya kufanya kazi) o List B (hati zinazoonyesha utambulisho wako) o List C (hati zinazoonyesha ruhusa ya kufanya kazi) • Ni lazima umuonyeshe mwajiri wako chaguo lako la aidha: o Hati moja ya List A au o Mchanganyiko wa hati moja ya List B na hati ya List C. • Kuna receipts (risiti) zilizoorodheshwa chini ya orodha za hati. Receipts pia zinakubalika kwa Form I-9 kwa vipindi tofauti vya muda. Una haki ya kuchagua hati zinazokubalika unazotaka kuonyesha kutoka kwa Form I-9 Lists of Acceptable Documents (Orodha ya Hati Zinazokubalika za Fomu I-9). Mwajiri wako haruhusiwi kukuhitaji uonyeshe hati maalum kulingana na hali yako kama mkimbizi au mhamaji au kulingana na asili yako ya kitaifa. Mwajiri ambaye anahitaji hati maalum anaweza kuwa anabagua kinyume cha sheria. Kwa mfano, ingawa unaweza kuwa na Hati ya Uidhinishaji wa Ajira (Employment Authorization Document, EAD), unaweza kuamua kuonyesha hati nyingine badala yake, kama vile kitambulisho cha serikali (hati ya List B) na kadi ya Ruzuku ya Serikali isiyo na kikomo (hati ya List C). .
Unaweza kuwa na aina kadhaa za hati zinazokubalika za Form I-9. • Unaweza kuonyesha I-94 kwa Form I-9. Utapata karatasi ya I-94 kutoka kwa Idara ya Usalama wa Ndani (Department of Homeland Security), kutoka kwenye tovuti ya Customs and Border Protection (Forodha na Ulinzi wa Mipaka). • Ikiwa wewe ni mkimbizi, I-94 ni receipt yako kwa hati ya List A ambayo ni halali kwa siku 90 kutoka siku yako ya kwanza ya kazi. Baada ya siku 90, lazima uonyeshe mwajiri wako ama EAD au mchanganyiko wa hati ya List B na kadi ya Ruzuku ya Serikali isiyo na kikomo. • Ikiwa wewe ni mhamaji, unaweza kutumia I-94 kama hati ya kudumu ya List C ambayo muda wake hauishi. • Wahamaji na wakimbizi wanastahiki kupata EAD. Ukiamua kuomba kuongezea muda EAD yako na maombi yako yawasilishwe kabla ya tarehe ya mwisho kwenye EAD yako, huenda ukaweza kuendelea kufanya kazi na EAD yako iliyopo. Kwa kipindi cha muda baada ya tarehe ya EAD yako kuisha muda, unaweza kuendelea kufanya kazi kwa kumwonyesha mwajiri wako EAD yako na notisi ya receipt ya I-797C (ikionyesha kwamba serikali ilipokea ombi lako la EAD mpya). Pigia simu Sehemu ya Haki za Wakimbizi na Wafanyakazi (Immigrant and Employee Rights Section, IER) kwa maelezo zaidi kuhusu uongezeaji muda otomatiki wa EAD. • Unaweza pia kuonyesha receipts za hati zilizopotea, kuharibika, au kuibiwa. Pindi tu unapoonyesha hati zako za kukamilisha Form I-9, mwajiri wako anaruhusiwa kukuuliza hati tena katika hali chache tu. • Sheria za wakati mwajiri lazima aombe hati tena zinajadiliwa katika Handbook for Employers M-274 (Kitabu cha Mwongozo wa Waajiri M-274). • Ikiwa ulionyesha EAD yako kwa Form I-9, mwajiri wako ataomba kuona hati nyingine kufikia wakati muda wa EAD yako kuisha ili kudhibitisha upya ruhusa yako ya kufanya kazi. Katia hatua hii, unaweza kuchagua kuonyesha hati ya List A au hati ya List C, kama vile kadi ya Ruzuku ya Serikali isiyo na kikomo. Unaweza kuchagua kuonyesha EAD mpya, lakini si lazima. • Iwapo ulionyesha kadi ya Ruzuku ya Serikali isiyo na kikomo kwa Section 2 kama uthibitisho wa ruhusa yako ya kufanya kazi na ukaweka "N/A" kwa tarehe ya muda kuisha katika Section 1, mwajiri wako haruhusiwi kukuomba utoe hati zaidi.
• Waajiri wanaoomba hati wakati hawapaswi kufanya hivyo, kwa msingi wa hali yako kama mhamaji au mkimbizi au kwa msingi wa asili yako ya kitaifa wanaweza kuwa wanakiuka sheria. Piga simu Sehemu ya Haki za Wakimbizi na Wafanyakazi kwa maelezo zaidi kuhusu wakati mwajiri wako anaruhusiwa kukuomba utoe hati zaidi. Unaweza kufanya kazi unaposubiri nambari yako ya Ruzuku ya Serikali. • Ukipata kazi lakini bado huna nambari yako ya Ruzuku ya Serikali (Social Security Number, SSN), Usimamizi wa Ruzuku ya Serikali unawaagiza waajiri kwamba wafanyakazi wanaruhusiwa kufanya kazi wakisubiri SSN yao. • Lazima mwajiri wako akulipe kila wakati kwa kazi yoyote iliyokamilika, hata kama bado unasubiri nambari yako ya Ruzuku ya Serikali. • Iwapo huna nambari yako ya Ruzuku ya Serikali unapoanza kazi yako, acha wazi kisanduku cha nambari ya Ruzuku ya Serikali katika Form I-9 ya Section 1. • Iwapo mwajiri wako hutumia E-Verify, E-Verify huagiza waajiri kuchelewesha kuunda kesi ya E-Verify hadi utakapopokea nambari yako ya Ruzuku ya Serikali. Unaweza kufanya kazi wakati huu ikiwa umekamilisha Form I-9. Sheria za E-Verify huruhusu kighairi hiki hasa na huwapa waajiri maagizo ya kufungua kesi hiyo. Maelezo zaidi yanapatikana katika e-verify.gov. Ilirekebishwa mnamo Agosti 2023 (Inaendelea kwenye ukurasa unaofuata)
Wasiliana Nasi • Kwa msaada zaidi, piga simu kwa Sehemu ya Haki za Wakimbizi na Wafanyakazi ya Laini ya Simu ya Moja kwa moja ya Wafanyakazi nambari ya simu 1-800-255-7688 au 1-800-237-2515 kwa watu walio na ulemavu wa kusikia. o Usaidizi wowote kutoka kwetu haulipishwi. Simu zinaweza kutojulikana, na huduma za lugha ya bila malipo zinapatikana. • Kujifunza mengi, tembelea tovuti yetu • Ili kuripoti ubaguzi, tembelea justice.gov/crt/filing-charge
Wondering how this text applies to your situation?
Free consultation, no commitment
Describe your situation. Our team will contact you by email about your consultation.
Continue your research in ChatGPT or Claude
Connect Omnilex to search the legal corpus from your AI assistant.